VISHETI
Mahitaji:- Unga wa ngano kg 1 Mafuta ya kupikia lita 1 Siagi robo kg Nazi iliyo kunwa (machicha) susu kikombe Sukari nusu kg Iliki kijiko cha chai Backing powder vijiko viwili vya chai Maji kiasi Matayarisho:- Weka unga wako kwenye bakuli Weka nazi yako iliyokunwa (machicha) Weka iliki Weka siagi Weka backing powder Changanya mchanganyiko vyote vichanganyikie kwenye unga Weka maji kiasi kuchanganya upate donge la unga Maji yasiwe mengi unga ukatota Kanda unga kidogo tuu ili maji yachanganyike vizuri Unga ukisha kua mlaini kata kata madonge Sukuma madonge kwenye kibao cha chapati iwe kama chapati Sukuma na unga mkavu kidodo ili madonge yasishike kwenye kibao Chukua kisu ukate dizain ya visheti Bandika mafuta ya kula jikoni Yakipata moto kaanga visheti ulivyo katakata vivve na kupata rangi ya broun Jinsi ya kuandaa sukari Weka sukari kwenye sufuria Iroweshe na maji kidogo sana Bandika jikoni na moto mdogo sukari iy...