TAMBI ZA SUKARI

Mahitaji:-

  • Tambi
  • Sukari
  • Mafuta ya kula
  • Hiliki
  • Maji

Jinsi ya kupika:-

  • Bandika mafuta yapate moto
  • Kaanga tambi ziwe rangi ya udongo (broun)
  • Chuja mafuta pembeni tambi zikishakua za rangi ya udongo (broun)
  • Ukisha chuja mafuta weka maji kiasi yasiwe mengi 
  • Weka hiliki na sukari 
  • Punguza moto kisha funikia maji yakauke na tambi zikauke kuiva  
  • Kama maji yakikauka hazija iva ongeza maji kidogo kidogo mpaka ziive. 
  • Chunga usiweke maji mengi zikatota
  • Maji yakisha kaukia, tambi zikiiva zitakua tayari kuandaa kwa kula


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Biriani (Biryani)

VISHETI