Biriani (Biryani)

BIRIANI (BIRYANI)
Mahitaji:
  • -Mchele kg 1½
  • -Vitunguu maji vi 5 au zaidi
  • -Vitunguu swaumu 1
  • -Tangawizi mbichi
  • -Viazi vi 5
  • -Mafuta ya kupikia L1
  • -Jira ts 2
  • -Maziwa mgando (mtindi) ½ L
  • -Nyanya ya kopo (tomato pure)
  • -nyanya fresh 10
  • -Mdalasini ts 3 au zaidi
  • -Pilipilimanga ½ kijiko cha chai
  • -Nyama yoyote upendayo
  • -Karafuu ½ kijiko cha chai
  • -Chumvi


Maandalizi:
  • Osha nyama yako vizuri. Ikate saizi uipendayo, kisha weka mchanganyiko ufuatao kwa muda wa lisaa limoja ili viungo vikolee ndani ya nyama kabla ya kuanza kuipika. (Chumvi, hiliki, mdalasini, vitunguu swaumu, karafuu kwambali, pilipili manga na tangawizi)
  • Menya vitunguu maji, vioshe na ukatekate raundi nzuri nyembamba. Kaanga vitunguu kwenye mafuta mengi yaliyo chemka mpaka viwe brauni (brown) kisha viweke pembeni ukiwa unaandaa vitu vingine.
  • Menya viazi, vioshe vizuri na kata katikati, yani vitate mara mbili tuu usikate vidogo vidogo. vikaange viazi kwenye mafuta pia kama ulinyo kaanga vitunguu. vikiiva uviweke pembeni.

Jinsi ya kupika rojo ya biriani (biryani):

  • Chukua nyama uliyokua umeshaiweka viungo weka kwenye sufuria kwa kuanza kupika. 
  • Moto wa jiko usiwe mkali sana kwasababu rojo na nyama isishike chini, na pia usiwemdogo sana. 
  • Rojo usiiweke maji, moto wajiko uwe mzuri ili isishike chini.
  • Weka nyanya zako zilizokatwakatwa vipande vidogo vidogo, weka pia nyanya ya kopo (pure) iwe  inaivia kwenye nyama.
  • Mchanganyiko ukianza kuchemka weka maziwa ya mgando (mtindi) mpaka rojo iive na nyanya ziwe nyekundu.
  • Baada ya rojo kuiva unaweka vitunguu vyako na viazi ulivyokua umevikaanga na kufunikia kwa  muda wa dk 10.
  • Dk 10 zikiisha rojo yako itakua tayari.

wali:
  • Andaa wali wako kama kawaida ya kupika wali, unaweza ukatia zabibu kama utapenda na rangi ya chakula upande ili kuleta mvuto lakini sio lazima ni wewe upendavyo jinsi ya kuandaa wali wako.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TAMBI ZA SUKARI

VISHETI