Mahindi ya nazi

Mahindi ya nazi sio kazi kutengeneza ni rahisi sana. Ni vyema uwe na mahindi machanga au ambayo hayajakua magumu. 

Mahitaji:

  • Mahindi mabichi
  • Nazi (tui)
  • Chumvi
  • Maji

Jinsi ya kupika:
  • Chemsha maji yako pamoja na mahindi weka na chumvi.
  • Mahindi yako yakishaiva unaweka tui lako la nazi na kumbuka kulipooza likiwa jikoni ili tui lisikatike mpaka litakapoanza kuchemkia.
  • Subiri mpaka tui liive ni vizuri usubiri pia tui lianze kukaukia ili mahindi yakolee vizuri tui.
  • Baada ya hapo mahindi yatakua tayari kwa kuandaa.

NB:
  • Kwa wale wanaonunua mahindi yaliyokwisha chemshwa. 
  • Unabandika tuu tui lako, na mahindi yako mpaka lichemkie na likaukie bila kusahau chumvi maana maranyingi ukiweka tui linakua linanyonya ile chumvi kwenye mahindi iliyokuwepo sasa ni bora kuongeza.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TAMBI ZA SUKARI

Biriani (Biryani)

VISHETI