VISHETI
Mahitaji:-
- Unga wa ngano kg 1
- Mafuta ya kupikia lita 1
- Siagi robo kg
- Nazi iliyo kunwa (machicha) susu kikombe
- Sukari nusu kg
- Iliki kijiko cha chai
- Backing powder vijiko viwili vya chai
- Maji kiasi
Matayarisho:-
- Weka unga wako kwenye bakuli
- Weka nazi yako iliyokunwa (machicha)
- Weka iliki
- Weka siagi
- Weka backing powder
- Changanya mchanganyiko vyote vichanganyikie kwenye unga
- Weka maji kiasi kuchanganya upate donge la unga
- Maji yasiwe mengi unga ukatota
- Kanda unga kidogo tuu ili maji yachanganyike vizuri
- Unga ukisha kua mlaini kata kata madonge
- Sukuma madonge kwenye kibao cha chapati iwe kama chapati
- Sukuma na unga mkavu kidodo ili madonge yasishike kwenye kibao
- Chukua kisu ukate dizain ya visheti
- Bandika mafuta ya kula jikoni
- Yakipata moto kaanga visheti ulivyo katakata vivve na kupata rangi ya broun
- Weka sukari kwenye sufuria
- Iroweshe na maji kidogo sana
- Bandika jikoni na moto mdogo sukari iyayuke na yale maji yakauke
- Kisha tia visheti vilivyokaangwa na kuvirusha rusha ili kuvigeuza vya juu vije chini na vya chini vije juu sukari ienee kwenye visheti
- Sukari ikisha ingia vizuri katika visheti na kukauka, viweke kwenye sinia au tray vipowe tayari kwa kula
Jinsi ya kuandaa sukari
Maoni
Chapisha Maoni