SAMBUSA

Jinsi ya kupika sambusa
Mahitaji:
  • Nyama ya kusaga
  • Vitunguu maji
  • Vitunguu swaumu
  • Mdalasini
  • Jira
  • Hiliki
  • Chumvi
  • Tangawizi
  • Giligilani
  • Pilipili manga
  • Limao au ndimu
  • Pilipili ya kawaida ukipenda
  • Manda
  • Mafuta ya kupikia
  • Unga wa ngano
Maandalizi na upishi:
  • Chukua nyama ya kusaga na uchanganye viungo (vitunguu swaumu, mdalasini, jira, hiliki, chumvi, tangawizi, giligilani, pilipili manga, limao au ndimu na pilipili ya kawaida kama ukipenda.
  • Changanya vichanganyike na uiache vikolee kama muda walisaa.
  • Kata kata vitunguu maji saizi ndogo ndogo.
  • Weka mafuta kidogo kwenye kikaangio chako na uikaannge nyama, unaweza kuikaanga bila mafuta kama wewe sio mpenzi wa mafuta, mara nyingi nyama hua inamafuta mengi.
  • Nyama ikishakua ya brauni weka vitunguu maji ulivyo katakata.
  • Usiikaange sana ukishaweka vitunguu kisha iweke chini ipowe.
  • Nyama ikishapoa funga sambusa zako na manda gundi utatumia unga wa ngano.
  • Baada ya kuzifunga utazichoma kwenye mafuta mengi. 
  • Zikiwa brauni hapo utazitoa na zitakua tayari.
NB:
  • Gundi ya unga wa ngano ni rahisi kutengeneza, chukua unga kwenye kibakuli kidogo weka na maji koroga isiwe nyepesi sana itakua haishiki vizuri.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TAMBI ZA SUKARI

Biriani (Biryani)

VISHETI