Lasagne (Lazanya)
Lasagne (lazanya) ni chakula cha kitaliano. Ni rahisi kuandaa na kina ladha ya kipekee. Unaweza kuandaa kama chakula cha jioni (diner). Unaweza kuandaa na salad kama ukipenda. Mahitaji: Sosi; Nyama ya kusaga Vitunguu maji Vitunguu saumu Tangawizi Nyanya Chumvi Mafuta ya kupikia Hoho Karoti Lasagne (lazanya) Cream (samli ya maji) Biskuti za lazanya Cheese (jibini) Sosi ya nyama ya kusaga Mapishi ya sosi: Andaa sosi ya nyama ya kusaga, inapikwa kawaida Katakata vitunguu na kuvikaanga kwenye mafuta kama unapika mchuzi wa kawaida Vitunguu vikibadilika rangi na kuanza kua rangi ya udongo (broun) weka hoho na karoti, koroga kama dk 1 Weka nyama, vitunguu saumu na tangawizi. Changanya mpaka nyama ichambuke na kubadilika rangi kua ya udongo (broun) Weka nyanya, punguza moto kisha funikia nyanya iive. Usitie maji ili sosi iwe nzito isiwe maji kama mchuzi. Jinsi ya kuandaa lasagne (lazanya) Chukua tray au bakuli kubwa inayo ingia...