Lasagne (Lazanya)



Lasagne (lazanya) ni chakula cha kitaliano. Ni rahisi kuandaa na kina ladha ya kipekee. Unaweza kuandaa kama chakula cha jioni (diner). Unaweza kuandaa na salad kama ukipenda.

Mahitaji:

Sosi;
  • Nyama ya kusaga
  • Vitunguu maji 
  • Vitunguu saumu 
  • Tangawizi
  • Nyanya
  • Chumvi 
  • Mafuta ya kupikia
  • Hoho
  • Karoti
Lasagne (lazanya)
  • Cream (samli ya maji)
  • Biskuti za lazanya
  • Cheese (jibini)
  • Sosi ya nyama ya kusaga

Mapishi ya sosi:

  • Andaa sosi ya nyama ya kusaga, inapikwa kawaida 
  • Katakata vitunguu na kuvikaanga kwenye mafuta kama unapika mchuzi wa kawaida
  • Vitunguu vikibadilika rangi na kuanza kua rangi ya udongo (broun) weka hoho na karoti, koroga kama dk 1
  • Weka nyama, vitunguu saumu na tangawizi. Changanya mpaka nyama ichambuke na kubadilika rangi kua ya udongo (broun)
  • Weka nyanya, punguza moto kisha funikia nyanya iive. Usitie maji ili sosi iwe nzito isiwe maji kama mchuzi.

Jinsi ya kuandaa lasagne (lazanya)

Chukua tray au bakuli kubwa inayo ingia kwenye oven. Washa kabisa oven moto juu na chini 220c. Panga biskuti za lazanya chini, tandaza sosi ya nyama juu yake, kiasi tuu ili upate leya tatu au zaidi kama nyama itakua nyingi. Weka cheese (jibini) nayo itandaze juu yake. Kisha mwagia samli yako (cream) iliyokua ya maji. nikisema ya maji namaanisha inayofanana na tui la nazi. (Nitaweka picha ya hiyo samli kwa wasioelewe waone picha). Endelea kupanga leya ingine kwa kufuata mpangilio huo huo. (Angalia picha jinsi ya kupanga kama utakua haujaelewa). Kisha weka kwenye oven kwa muda wa dk 40. Tazama kama itakua imeiva, mimi hua naibonyeza kutumia uma kuona kama zile biskuti zimelainika na ile samli imekaukia. kisha najua kua imeiva. 
maandalizi ya sosi

jinsi ya kuanza kupanga lazanya kabla ya kuweka kwenye oven. na kile kiboksi ndio cha samli ya maji

leya ya kwanza imekamilika 

bakuli yangu imejaa na leya 3

lasagne ikiwa imeiva tayari kwa kuandaa

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TAMBI ZA SUKARI

Biriani (Biryani)

VISHETI