Egg chop

Mahitaji:

  • Viazi 7
  • Chumvi kijiko cha chai nusu
  • Mayai 10
  • Mafuta ya kula lita 1
  • Unga wa ngano nusu kibakuli

Mapishi:

  • Chemsha viazi vyote, chumvi na mayai 8
  • Mayai na viazi vikiiva weka mayai pembeni chuja maji yote kisha uponde ponde viazi mpaka vipondeke viwe laini
  • Menya mayai yaliyo chemshwa 
  • Chukua yai moja moja zungushia viazi juu mpaka upate mduara mzuri kisha zungushia unga wa ngano ili viazi visivurugike ukiwa unakaanga (angalia picha jinsi nilivyo zungushia yai ndangi viazi juu)
  • Andaa ute wa yai (white egg)
  • Weka mafuta jikoni ya chemke
  • Chovea maduara yako kwenye ute wa mayai (white egg) kisha ukaange kwenye mafuta
  • Zikiiva tayari kuandaa
Jinsi ya kuzungushia viazi na unga juu, ndani ni yai la kuchemsha
Tayari kwa kula
Ndani

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

TAMBI ZA SUKARI

Biriani (Biryani)

VISHETI