MAKANDE
Mahitaji: Mahindi yaliyo kobolewa Maharage Chumvi Tui la nazi Kitunguu nusu Nyanya moja Mapishi: Chemsha mahindi, maharage na chumvi mpaka yaive. Katia kitunguu na nyanya kwenye mchemsho wako. Kitunguu na nyanya kikiiva weka tui la nazi na likiiva chakula chako kitakua tayari. NB: Unaweza weka magadi kwenye kuchemsha mahindi na maharage lakini sio lazima. Magadi yanasaidia mahindi na maharage kuiva haraka. mahindi ya kukoboa makande yakiwa tayari