Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2017

SAMBUSA

Picha
Jinsi ya kupika sambusa Mahitaji: Nyama ya kusaga Vitunguu maji Vitunguu swaumu Mdalasini Jira Hiliki Chumvi Tangawizi Giligilani Pilipili manga Limao au ndimu Pilipili ya kawaida ukipenda Manda Mafuta ya kupikia Unga wa ngano Maandalizi na upishi: Chukua nyama ya kusaga na uchanganye viungo (vitunguu swaumu, mdalasini, jira, hiliki, chumvi, tangawizi, giligilani, pilipili manga, limao au ndimu na pilipili ya kawaida kama ukipenda. Changanya vichanganyike na uiache vikolee kama muda walisaa. Kata kata vitunguu maji saizi ndogo ndogo. Weka mafuta kidogo kwenye kikaangio chako na uikaannge nyama, unaweza kuikaanga bila mafuta kama wewe sio mpenzi wa mafuta, mara nyingi nyama hua inamafuta mengi. Nyama ikishakua ya brauni weka vitunguu maji ulivyo katakata. Usiikaange sana ukishaweka vitunguu kisha iweke chini ipowe. Nyama ikishapoa funga sambusa zako na manda gundi utatumia unga wa ngano. Baada ya kuzifunga utazichoma kwenye mafuta mengi.  Zikiwa brauni

Mahindi ya nazi

Picha
Mahindi ya nazi sio kazi kutengeneza ni rahisi sana. Ni vyema uwe na mahindi machanga au ambayo hayajakua magumu.  Mahitaji: Mahindi mabichi Nazi (tui) Chumvi Maji Jinsi ya kupika: Chemsha maji yako pamoja na mahindi weka na chumvi. Mahindi yako yakishaiva unaweka tui lako la nazi na kumbuka kulipooza likiwa jikoni ili tui lisikatike mpaka litakapoanza kuchemkia. Subiri mpaka tui liive ni vizuri usubiri pia tui lianze kukaukia ili mahindi yakolee vizuri tui. Baada ya hapo mahindi yatakua tayari kwa kuandaa. NB: Kwa wale wanaonunua mahindi yaliyokwisha chemshwa.  Unabandika tuu tui lako, na mahindi yako mpaka lichemkie na likaukie bila kusahau chumvi maana maranyingi ukiweka tui linakua linanyonya ile chumvi kwenye mahindi iliyokuwepo sasa ni bora kuongeza.

Biriani (Biryani)

Picha
BIRIANI (BIRYANI) Mahitaji: -Mchele kg 1½ -Vitunguu maji vi 5 au zaidi -Vitunguu swaumu 1 -Tangawizi mbichi -Viazi vi 5 -Mafuta ya kupikia L1 -Jira ts 2 -Maziwa mgando (mtindi) ½ L -Nyanya ya kopo (tomato pure) -nyanya fresh 10 -Mdalasini ts 3 au zaidi -Pilipilimanga ½ kijiko cha chai -Nyama yoyote upendayo -Karafuu ½ kijiko cha chai -Chumvi Maandalizi: Osha nyama yako vizuri. Ikate saizi uipendayo, kisha weka mchanganyiko ufuatao kwa muda wa lisaa limoja ili viungo vikolee ndani ya nyama kabla ya kuanza kuipika. (Chumvi, hiliki, mdalasini, vitunguu swaumu, karafuu kwambali, pilipili manga na tangawizi) Menya vitunguu maji, vioshe na ukatekate raundi nzuri nyembamba. Kaanga vitunguu kwenye mafuta mengi yaliyo chemka mpaka viwe brauni (brown) kisha viweke pembeni ukiwa unaandaa vitu vingine. Menya viazi, vioshe vizuri na kata katikati, yani vitate mara mbili tuu usikate vidogo vidogo. vikaange viazi kwenye mafuta pia kama ulinyo kaanga vitunguu. vikiiva

Karibu

Habari! hii ni mara yangu ya kwanza kufungua blog. Sababu iliyonipelekea kufungua blog hii ni ningependelea niwe naweka mapishi mbalimbali ili niweze kujumuika na wenzangu wanaopenda kupika. Blog hii nitakua nikituma jinsi ya kupika kwa kiswahili. Ni matunaini yangu mtapendelea mapishi yangu na kufurahia, karibuni sana.