Hii ilikua kwa sherehe ya kuzaliwa ya mtoto wangu alipotimiza miaka minne. kama kuna atakaependa kujua jinsi ya kutengeneza keki hii, weka comment. ni rahisi sana na haina garama.
Mahitaji : - Tambi Sukari Mafuta ya kula Hiliki Maji Jinsi ya kupika:- Bandika mafuta yapate moto Kaanga tambi ziwe rangi ya udongo (broun) Chuja mafuta pembeni tambi zikishakua za rangi ya udongo (broun) Ukisha chuja mafuta weka maji kiasi yasiwe mengi Weka hiliki na sukari Punguza moto kisha funikia maji yakauke na tambi zikauke kuiva Kama maji yakikauka hazija iva ongeza maji kidogo kidogo mpaka ziive. Chunga usiweke maji mengi zikatota Maji yakisha kaukia, tambi zikiiva zitakua tayari kuandaa kwa kula
BIRIANI (BIRYANI) Mahitaji: -Mchele kg 1½ -Vitunguu maji vi 5 au zaidi -Vitunguu swaumu 1 -Tangawizi mbichi -Viazi vi 5 -Mafuta ya kupikia L1 -Jira ts 2 -Maziwa mgando (mtindi) ½ L -Nyanya ya kopo (tomato pure) -nyanya fresh 10 -Mdalasini ts 3 au zaidi -Pilipilimanga ½ kijiko cha chai -Nyama yoyote upendayo -Karafuu ½ kijiko cha chai -Chumvi Maandalizi: Osha nyama yako vizuri. Ikate saizi uipendayo, kisha weka mchanganyiko ufuatao kwa muda wa lisaa limoja ili viungo vikolee ndani ya nyama kabla ya kuanza kuipika. (Chumvi, hiliki, mdalasini, vitunguu swaumu, karafuu kwambali, pilipili manga na tangawizi) Menya vitunguu maji, vioshe na ukatekate raundi nzuri nyembamba. Kaanga vitunguu kwenye mafuta mengi yaliyo chemka mpaka viwe brauni (brown) kisha viweke pembeni ukiwa unaandaa vitu vingine. Menya viazi, vioshe vizuri na kata katikati, yani vitate mara mbili tuu usikate vidogo vidogo. vikaange viazi kwenye mafuta pia kama ulinyo kaanga vitunguu. vikiiva ...
Mahitaji: Mahindi yaliyo kobolewa Maharage Chumvi Tui la nazi Kitunguu nusu Nyanya moja Mapishi: Chemsha mahindi, maharage na chumvi mpaka yaive. Katia kitunguu na nyanya kwenye mchemsho wako. Kitunguu na nyanya kikiiva weka tui la nazi na likiiva chakula chako kitakua tayari. NB: Unaweza weka magadi kwenye kuchemsha mahindi na maharage lakini sio lazima. Magadi yanasaidia mahindi na maharage kuiva haraka. mahindi ya kukoboa makande yakiwa tayari
Maoni
Chapisha Maoni