Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2017

MAKANDE

Picha
Mahitaji: Mahindi yaliyo kobolewa Maharage  Chumvi Tui la nazi  Kitunguu nusu Nyanya moja  Mapishi: Chemsha mahindi, maharage na chumvi mpaka yaive. Katia kitunguu na nyanya kwenye mchemsho wako. Kitunguu na nyanya kikiiva weka tui la nazi na likiiva chakula chako kitakua tayari. NB:   Unaweza weka magadi kwenye kuchemsha mahindi na maharage lakini sio lazima. Magadi yanasaidia mahindi na maharage kuiva haraka. mahindi ya kukoboa makande yakiwa tayari

VIAZI VYA OVEN

Picha
MAHITAJI: Viazi Vitunguu maji Uyoga Karoti Hoho Chumvi Mmafuta ya kupikia Nyama ya kuku, ngòmbe au samaki MAANDALIZI: Washa oven 200° Menya vitu vyako vyote, osha vizuri na kukata viazi katikati (mara mbili) na vingine katakata vidogo vidogo kama utakavyoona kwenye picha. Chukua tray au bakuli inayoingia kwenye oven kisha weka mchanganyiko wote wa mboga, viazi na nyama kisha mwagia mafuta kidogo juu yake. Weka kwenye oven kwa muda wa dk 45 kisha tayari kwa kuandaa kula. maandalizi tayari kwa kuweka kwenye oven tayari kwa kula

Lasagne (Lazanya)

Picha
Lasagne (lazanya) ni chakula cha kitaliano. Ni rahisi kuandaa na kina ladha ya kipekee. Unaweza kuandaa kama chakula cha jioni (diner). Unaweza kuandaa na salad kama ukipenda. Mahitaji: Sosi; Nyama ya kusaga Vitunguu maji  Vitunguu saumu  Tangawizi Nyanya Chumvi  Mafuta ya kupikia Hoho Karoti Lasagne (lazanya) Cream (samli ya maji) Biskuti za lazanya Cheese (jibini) Sosi ya nyama ya kusaga Mapishi ya sosi: Andaa sosi ya nyama ya kusaga, inapikwa kawaida  Katakata vitunguu na kuvikaanga kwenye mafuta kama unapika mchuzi wa kawaida Vitunguu vikibadilika rangi na kuanza kua rangi ya udongo (broun) weka hoho na karoti, koroga kama dk 1 Weka nyama, vitunguu saumu na tangawizi. Changanya mpaka nyama ichambuke na kubadilika rangi kua ya udongo (broun) Weka nyanya, punguza moto kisha funikia nyanya iive. Usitie maji ili sosi iwe nzito isiwe maji kama mchuzi. Jinsi ya kuandaa lasagne (lazanya) Chukua tray au bakuli kubwa inayo ingia...

Egg chop

Picha
Mahitaji: Viazi 7 Chumvi kijiko cha chai nusu Mayai 10 Mafuta ya kula lita 1 Unga wa ngano nusu kibakuli Mapishi: Chemsha viazi vyote, chumvi na mayai 8 Mayai na viazi vikiiva weka mayai pembeni chuja maji yote kisha uponde ponde viazi mpaka vipondeke viwe laini Menya mayai yaliyo chemshwa  Chukua yai moja moja zungushia viazi juu mpaka upate mduara mzuri kisha zungushia unga wa ngano ili viazi visivurugike ukiwa unakaanga (angalia picha jinsi nilivyo zungushia yai ndangi viazi juu) Andaa ute wa yai (white egg) Weka mafuta jikoni ya chemke Chovea maduara yako kwenye ute wa mayai (white egg) kisha ukaange kwenye mafuta Zikiiva tayari kuandaa Jinsi ya kuzungushia viazi na unga juu, ndani ni yai la kuchemsha Tayari kwa kula Ndani

VISHETI

Picha
Mahitaji:- Unga wa ngano kg 1 Mafuta ya kupikia lita 1 Siagi robo kg Nazi iliyo kunwa (machicha) susu kikombe Sukari nusu kg Iliki kijiko cha chai Backing powder vijiko viwili vya chai Maji kiasi Matayarisho:- Weka unga wako kwenye bakuli  Weka nazi yako iliyokunwa (machicha) Weka iliki Weka siagi Weka backing powder Changanya mchanganyiko vyote vichanganyikie kwenye unga Weka maji kiasi kuchanganya upate donge la unga Maji yasiwe mengi unga ukatota Kanda unga kidogo tuu ili maji yachanganyike vizuri Unga ukisha kua mlaini kata kata madonge  Sukuma madonge kwenye kibao cha chapati iwe kama chapati Sukuma na unga mkavu kidodo ili madonge yasishike kwenye kibao Chukua kisu ukate dizain ya visheti  Bandika mafuta ya kula jikoni Yakipata moto kaanga visheti ulivyo katakata  vivve na kupata rangi ya broun  Jinsi ya kuandaa sukari Weka sukari kwenye sufuria Iroweshe na maji kidogo sana  Bandika jikoni na moto mdogo sukari iy...

TAMBI ZA SUKARI

Picha
Mahitaji : - Tambi Sukari Mafuta ya kula Hiliki Maji Jinsi ya kupika:- Bandika mafuta yapate moto Kaanga tambi ziwe rangi ya udongo (broun) Chuja mafuta pembeni tambi zikishakua za rangi ya udongo (broun) Ukisha chuja mafuta  weka maji kiasi yasiwe mengi  Weka hiliki na sukari  Punguza moto kisha funikia maji yakauke na tambi zikauke kuiva   Kama maji yakikauka hazija iva ongeza maji kidogo kidogo mpaka ziive.  Chunga usiweke maji mengi zikatota Maji yakisha kaukia, tambi zikiiva zitakua tayari kuandaa kwa kula

Budapest rull (Swissrull marengs) ya matunda na nuts

Picha
Budapest ni cake ya marings, almond na matunda ni rahisi kutengeneza na haichukui muda mrefu. Mahitaji: Ute wa mayai 6 Sukari dl 3 Vanila sauce ya unga pakt 1 Matunda yoyote upendayo Almond 200g Cream boksi moja Matayarisho: - Washa oven ipatemoto wa 170 C  -  Saga ute wa mayai yako, sukari na vanila sauce kwa kutumia mix    mpaka iwe marings - Saga almond pembeni na usizisage sana zisiwe unga - Andaa pan yako ya (30-40cm) utakayoweka kwenye oven - Weka kwenye pan yako ya (30-40cm) mchanganyiko uliosanga wa ute na sukari na mwagia almond zako kwa juu ya ule mchanganyiko sambaza kote juu ya pan kisha weka ndani ya oven kwa muda wa dk 20 hadi 22 -Baada ya dk 20-22 toa wacha ipowe kicha igeuze juu chini kwa kutumia karatasi lililo saizi na hy keki kuzuie zile almond zisimwagike -Saga cream yako mpaka iwe povu zito kisha mwagia pale juu ya keki uliokwisha igeuza juu chini weka matunda yako uliyokatakata saizi ndogondogo -Zungusha (roll)...

Vanila cake

Picha
Hii ilikua kwa sherehe ya kuzaliwa ya mtoto wangu alipotimiza miaka minne. kama kuna atakaependa kujua jinsi ya kutengeneza keki hii, weka comment. ni rahisi sana na haina garama.

SAMBUSA

Picha
Jinsi ya kupika sambusa Mahitaji: Nyama ya kusaga Vitunguu maji Vitunguu swaumu Mdalasini Jira Hiliki Chumvi Tangawizi Giligilani Pilipili manga Limao au ndimu Pilipili ya kawaida ukipenda Manda Mafuta ya kupikia Unga wa ngano Maandalizi na upishi: Chukua nyama ya kusaga na uchanganye viungo (vitunguu swaumu, mdalasini, jira, hiliki, chumvi, tangawizi, giligilani, pilipili manga, limao au ndimu na pilipili ya kawaida kama ukipenda. Changanya vichanganyike na uiache vikolee kama muda walisaa. Kata kata vitunguu maji saizi ndogo ndogo. Weka mafuta kidogo kwenye kikaangio chako na uikaannge nyama, unaweza kuikaanga bila mafuta kama wewe sio mpenzi wa mafuta, mara nyingi nyama hua inamafuta mengi. Nyama ikishakua ya brauni weka vitunguu maji ulivyo katakata. Usiikaange sana ukishaweka vitunguu kisha iweke chini ipowe. Nyama ikishapoa funga sambusa zako na manda gundi utatumia unga wa ngano. Baada ya kuzifunga utazichoma kwenye mafuta mengi.  Zikiwa br...

Mahindi ya nazi

Picha
Mahindi ya nazi sio kazi kutengeneza ni rahisi sana. Ni vyema uwe na mahindi machanga au ambayo hayajakua magumu.  Mahitaji: Mahindi mabichi Nazi (tui) Chumvi Maji Jinsi ya kupika: Chemsha maji yako pamoja na mahindi weka na chumvi. Mahindi yako yakishaiva unaweka tui lako la nazi na kumbuka kulipooza likiwa jikoni ili tui lisikatike mpaka litakapoanza kuchemkia. Subiri mpaka tui liive ni vizuri usubiri pia tui lianze kukaukia ili mahindi yakolee vizuri tui. Baada ya hapo mahindi yatakua tayari kwa kuandaa. NB: Kwa wale wanaonunua mahindi yaliyokwisha chemshwa.  Unabandika tuu tui lako, na mahindi yako mpaka lichemkie na likaukie bila kusahau chumvi maana maranyingi ukiweka tui linakua linanyonya ile chumvi kwenye mahindi iliyokuwepo sasa ni bora kuongeza.

Biriani (Biryani)

Picha
BIRIANI (BIRYANI) Mahitaji: -Mchele kg 1½ -Vitunguu maji vi 5 au zaidi -Vitunguu swaumu 1 -Tangawizi mbichi -Viazi vi 5 -Mafuta ya kupikia L1 -Jira ts 2 -Maziwa mgando (mtindi) ½ L -Nyanya ya kopo (tomato pure) -nyanya fresh 10 -Mdalasini ts 3 au zaidi -Pilipilimanga ½ kijiko cha chai -Nyama yoyote upendayo -Karafuu ½ kijiko cha chai -Chumvi Maandalizi: Osha nyama yako vizuri. Ikate saizi uipendayo, kisha weka mchanganyiko ufuatao kwa muda wa lisaa limoja ili viungo vikolee ndani ya nyama kabla ya kuanza kuipika. (Chumvi, hiliki, mdalasini, vitunguu swaumu, karafuu kwambali, pilipili manga na tangawizi) Menya vitunguu maji, vioshe na ukatekate raundi nzuri nyembamba. Kaanga vitunguu kwenye mafuta mengi yaliyo chemka mpaka viwe brauni (brown) kisha viweke pembeni ukiwa unaandaa vitu vingine. Menya viazi, vioshe vizuri na kata katikati, yani vitate mara mbili tuu usikate vidogo vidogo. vikaange viazi kwenye mafuta pia kama ulinyo kaanga vitunguu. vikiiva ...

Karibu

Habari! hii ni mara yangu ya kwanza kufungua blog. Sababu iliyonipelekea kufungua blog hii ni ningependelea niwe naweka mapishi mbalimbali ili niweze kujumuika na wenzangu wanaopenda kupika. Blog hii nitakua nikituma jinsi ya kupika kwa kiswahili. Ni matunaini yangu mtapendelea mapishi yangu na kufurahia, karibuni sana.